Friday, December 17, 2010

UTAGUNDUAJE KAMA UNA MIMBA CHANGA? SEHEMU YA1.

Mara nyingi ni vigumu mwanamke kugundua kama ameshika mimba siku za mwanzoni hadi pale anapokosa kuona siku zake za hedhi. pamoja na ugumu huo kuna dalili ambazo zinaweza kufanya uhisi kama una mimba katika siku za mwanzoni ambazo ni kuanzia  siku ya 18 toka mimba itungwe.

Dalili hizi zinatofautiana kwa kila mtu, wapo ambao wanaweza kuzipata zote na ambao hupata baadhi tu ya dalili hizi na pia wapo ambao hawazipati kabisa.

Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na:

1.JOTO LA MWILI KUPANDA.(basal body temperature stay high)

   Wanawake wengi hushindwa kutambua dalili hii pale wanapoipata kutokana na kutokuwa na uelewa
    juu ya miili yao.
    Hali hii inaonekana katika siku za mwanzo ambambo huweza kudumu kwa muda mrefu kiasi hivyo
    kama itadumu zaidi ya siku 18 basi ni vizuri kupima ili kujua kama inatokana na ujauzito au la.

2. KUPATA HAJA NDOGO MARA KWA MARA.(frequent urination)
    Kubanwa na haja ndogo mara kwa mara pia inaweza ikawa ni dalili mojawapo ya kuwa na mimba
    changa.

3.KUWA MWEPESI KUHISI HARAFU YA VITU  MBALI MBALI HASA  HARUFU MBAYA.(sensitivity to odors)
   Wakati wa mimba changa wanawake wengi wanakuwa wepesi wa kuhisi harufu ya vitu mbali mbali hasa zile harufu zisizo za kupendeza na kumfanya achukie vitu vingi vyenye kutoa harufu hizo.
 wakati kama huu si ajabu ukaona mtu hataki mume wake amsogelee kwa kudai anatoa harufu mbaya.
ukiona dalili kama hii inaweza ikawa ni ishara ya kuwa mjamzito hivyo unapaswa kufanya uchunguzi.

4.KUKOSA HEDHI.(missed period)
  Kwa kawaida mama mjamzito hapati siku zake za hedhi isipokua anaweza akapatwa na hali ya kuvuja kunakofanana na ile ya hedhi ila damu yake huwa nyepesi sana na hudumu kwa muda mfupi kati ya siku1 au 2 (implantation bleeding) hivyo    unapokosa kuona siku zako za hedhi
  unapaswa kuchunguza sababu za kukosekana kwa hedhi.

5. KICHEFU CHEFU AU KUTAPIKA.( Nausea or vomiting).

11 comments:

  1. samahani, mimi naitwa Amina nina miaka 24 lakini sasa umefika wakati nahitaji mtoto kama maridhiano mimi na mchumba wangu lakini sasa nashindwa kuelewa siku halali za kusika mimba sababu mzunguko wangu ulikuwa unaenda vizuri lakini sasa umebadilika mwezi April niliona kuanzia tarehe 18 lakini sasa mwezi May nikaanza kuona tarehe 16-20 sasa je hapo nilenge wapi mana nimeanza kukutana na mwenzangu tarehe 26-27 je katika tarehe hizo kuna uwezekano wa mimba

    ReplyDelete
  2. Mimi naitwa Monica, ninamiezi 6 kwenye ndoa,sijabahatika bado kupata mtoto, ila pia mzunguko wangu siuelewi vizuri kwasababu unabadilika badilika mara kwa Mara, mara ya mwisho kupata damu ni December 9, na Leo tar.12mwezi wa kwanza nimepata nyingine tena, na nimekutana na mmewangu tar.27,1 na tar.11 January 2016. Sasa sijajua siku rasmi ya kushika mimba ni IPI kati ya izo? Pia mwanamke akiwa na mzunguko wa siku 35 siku rasmi ya kushika mimba ni ipi? Na pia kunauwezekano kwa mwanamke anaepatwa na hedhi akakosa mtoto?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nipigie kwa namba yangu nikuelekeze 0625 490 456

      Delete
    2. Nipigie kwa namba yangu nikuelekeze 0625 490 456

      Delete
    3. Mambo Irene napenda kujua kama ulisaidika kwa ushauri wa Dr.

      Delete
    4. Nina ndugu yangu na yy anashida kama yako hivyo ninaomba msaada kama hutojali

      Delete
  3. Hellow,doctor Mimi Matti yangu yamejaa na yananiuma sana,pia tumbo linauma na kuacha ni kama lile la period ila sijielew sijawahi kujiona hivi

    ReplyDelete
  4. Naitwa Imelda mm sijaingia period mwezi wa kumi namoja ilitakiwa niingie tarehe1 ila imepita nanimepima mimba mara 3 ni negative.matiti yamejaa nayanauma nanilifanya tendo siku zahatari je shida itakuwa wapi

    ReplyDelete
  5. Mlango wa uzazi unajifunga baada ya muda gani mara tu mbegu za kiume kuingia ndani kwenda kurutubisha yai??

    ReplyDelete
  6. Mmmmh hii Kali tupeni majib madaktar tunawategemea nyinyi

    ReplyDelete