Thursday, February 3, 2011

MAGONJWA YA NGONO

 Napenda kuchukua nafasi hii kuwataka radhi wapendwa wafuatiliaji wa blog hii kwa ukimya uliojitokeza kati kati ya Mwezi Desemba na january mwaka huu, hiyo yote ni kutokana na majukumu ya kujenga Taifa yaliyonibana kwa kipindi hicho.

Ikiwa ni siku ya 34 toka mwaka huu wa 2011 uannze ninayofuraha kubwa kuwajulisheni kuwa mwaka huu hautakuwa kama mwaka uliyopita kwani mtapata vitu adimu na vitamu kwa wakati muafaka.

Nimerejea uwanjani na Gunia zima la utirio hivyo mkae mkao wa kula.

Baada ya kuwadokeza hayo, sasa tuingie moja kwa moja katika mada yetu hapo juu, kwa kifupi tu ni kwamba ili mtu awe na uzazi salama anapaswa kujua yale mambo yanayoweza kuathiri mfumo wake wa uzazi ili kuweza kujiepusha nayo.

Mfumo wa uzazi unaweza kuathiria na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya ngono ambayo hushambulia mfumo huo, leo tutajadili baadhi ya magonjwa hayo ambapo tutapata kujua majina yao, jinsi yanavyoambukizwa, dalili na kinga au tiba zao ijapokuwa kipengele cha tiba sitakiongelea kwa undani.

1. KISONONO:
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi na hushambulia zaidi sehemu za siri za jinsia zote.

Dalili;
Dalili kuu za ugonjwa huu ni mgonjwa kutokwa na usaa kwenye sehemu za siri na mgonjwa kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo, na ukikaa kwa muda mrefu bila kutibiwa huenea zaidi kwenye viungo vingine vya uzazi.

Kuzuia/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni kuacha kujamiiana au kutumia kondom kwa kila tendo la ngono.
na kwa wale ambao tayari wanamaambukizi wanashauriwa kutibiwa wote hospitalini na kuacha kufanya ngono hadi wapone.


2. KASWENDE:
Huu ni ugonjwa wa ngono unaosababishwa na bakteria.

Dalili;
Mgonjwa wa Kaswende hupata mwasho mkali sehemu za siri na kupata vijeraha vidogo vidogo sehemu hizo na akikaa sana na ugonjwa huo bila kutibiwa huweza kuathirika sehemu zingine za mwili kama vile, Moyo, ubongo na hatimaye kusababisha kifo.

Kinga/ Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni; kuacha kujamiiana na ukishindwa kuacha kabisa basi fanya ngono iliyo salama(yaani utumie Condom)

Ugonjwa huu hutibiwa Hospitalini na inashauriwa  wenza wenye ugonjwa huu watibiwe kwa pamoja.
Wakati wa matibabu maswala ya kujamiiana yawekwe kando hadi matibabu yakamilike kwani yanaweza yakaongeza maambukizi mapya.

3. KLAMEDIA:
Huu ni mojawapo ya magonjwa ya ngono ambao haujafahamika unaambukizwa na wadudu wa aina gani.

Dalili;
Mgonjwa wa klamedia hutokwa na uchafu  katika sehemu zake za siri na kupata maumivu makali wakati wa haja ndogo na wakati wa kujamiiana.

Kinga/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni sawa na kinga ya magonjwa mengine ya zinaa, ili usiupate ugonjwa huu unashauriwa kuacha kabisa kufanya ngono au kutumia condom kwa kila tendo la ndoa.

Hugonjwa huu pia hutibiwa hospitalini.

4. TRIKOMONA:
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa (trikomonasi vaginalis) ambazo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Dalili;
Dalili za ugonjwa huu hutofautiana kwa kila jinsia.
WANAWAKE: Wanawake wenye ugonjwa huu hupatwa mwasho mkali  katika sehemu za siri,
                           Hutokwa na uchafu wa rangi ya njano au kijani wenye harufu mbaya sehemu za siri.

WANAUME:    Wanaume wenye ugonjwa huu hupata maumivu makali wakati wa haja ndogo.

Kinga/ Tiba;
Ugonjwa huu pia unazuilika kwa kuacha kujamiiana au kutumia condom kwa kila tendo la ngono.
Mgonjwa atatibiwa hospitalini na kupona kabisa.


5.UKIMWI:

No comments:

Post a Comment